The House of Favourite Newspapers

Ligi Kuu Bara 2019/20 Hatarini Kufutwa

0

KAMA janga la Virusi vya Corona halitakuwa na ahueni, basi upo uwezekano mkubwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu ukafutwa. Hiyo ikiwa ni wiki chache tangu serikali kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kusimamisha michezo yote ili kuepusha maambukizi hayo ya Virusi vya Corona.

 

Hadi ligi inasimamishwa, Simba walikuwa wanaongoza katika msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 71, Azam FC (54), Yanga (51), Namungo FC (50) na Coastal Union (46).

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, shirikisho hilo limeweka malengo kuhakikisha ligi inamalizika Juni 30, mwaka huu na kama ikifi kia hadi siku hiyo bado janga hilo halijapata ahueni, basi ligi itafutwa msimu huu.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa virusi hivyo ndiyo vimesababisha kusogezwa mbele muda wa kumalizika ligi hiyo kutoka Mei 30 hadi Juni 30, mwaka huu.

“Changamoto ya janga la Corona, ndiyo imesababisha kusogeza mbele muda wa kumalizika ligi hiyo kutoka Mei 30 hadi Juni 30, mwaka huu.

 

“Kama ikifi kia hadi Juni 30, mwaka huu janga hilo halitakuwa na ahueni, basi upo uwezekano wa ligi hiyo kufutwa na kusubiria kuanza kwa msimu mwingine mpya,” alisema mtoa taarifa huyo. Alipotafutwa Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao kuzungumzia hilo alisema: “Maamuzi yoyote ya ligi yataamuliwa na Kamati ya Utendaji ya TFF.”

Leave A Reply