The House of Favourite Newspapers

Linah Aanika Kisa cha Kuwa Bonge Nyanya

MKALI kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Esterlina Sanga ‘Linah’ amefungukia sababu ya kuwa mnene kupitiliza ‘bonge nyanya’ kiasi cha kusababisha mijadala mbalimbali katika mitandao ya kijamii.

Akipiga stori na Global TV katikati mwa wiki hii, Linah ameweka wazi sababu iliyomfanya kuwa mnene ni kutokana na kutoka kwenye uzazi hali iliyomfanya mwili na nafsi yake kuridhika na kujikuta bonge nyanya.

“Nimetoka kwenye kipindi kifupi mno cha uzazi, hii ndio sababu kubwa iliyonifanya niwe bonge, baada ya kujifungua mtoto nafsi na mwili wangu viliridhika, ndio maana nimekuwa na mwili mkubwa na wenye afya,” alisema Linah.

ALLY KATALAMBULA | IJUMAA

Comments are closed.