The House of Favourite Newspapers

Linah Anaswa Nusu Mtupu

0

Musa Mateja

Msanii wa muziki Bongo, Estelina Sanga ‘Linah’, juzikati alitinga kigauni kilichomuacha nusu utupu, hali iliyomfanya azodolewe. Mwanadada huyo alivaa kivazi hicho kwenye pati iliyoandaliwa na msanii mwenzake Zuena Mohammed ‘Shilole’ nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar ya kumpongeza Mheshimiwa John Magufuli aliyechaguliwa kuwa rais wa Tanzania.

Bila aibu Linah alionekana akikatiza huku na kule na mara kadhaa kigauni hicho kilikuwa kikipanda juu na kuiacha sehemu kubwa ya mapaja yake nje, hivyo kuibua minong’ono.

“Mh! Huyu binti sasa kapinda, lile ndiyo vazi gani sasa, ile yote kuwatega wanaume tu wakati ana mtu wake,” alisema mdau mmoja aliyekuwa ukumbini hapo.

Leave A Reply