The House of Favourite Newspapers

Linah Kivazi Chake Chazua Gumzo

0

LINAH (1)    Esterina Sanga ‘Linah’

MWANDISHI WETU

KIVAZI cha staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Esterina Sanga ‘Linah’ alichokivaa usiku wa shoo ya Black Tie iliyofanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa King Solomon, Dar kiligeuka gumzo kwa kuongelewa na baadhi ya watu waliohudhuria shoo hiyo.

LINAH (2)Katika shoo hiyo iliyokuwa maalum kwa King of The Best Melodies, Christian Bella aliyekuwa akitimiza miaka 10 tangu kuanza kwa muziki nchini, Linah alitinga ukumbini hapo na kivazi hicho cheusi chenye nakshinakshi eneo la mbele huku miguuni akiwa na viatu virefu vyenye kamba nyeupe hadi mapajani.

LINAH (3)“Duh! Huyu si Linah? Hii kiboko, sijawahi ona kivazi amaizing kama hiki,” alisikika mdada mmoja aliyekuwa karibu na Linah na kuongeza;

LINAH (4)“Da! Leo katokelezea kama mastaa wa mamtoni akina Amber Rose na Kim Kardashian.

Baada ya Linah kutoka ‘red carpet’ paparazi wetu alimfuata kujua machache juu ya kivazi hicho ambapo alifunguka;

LINAH (5)“Mara nyingi ninapotoka kwenye shoo kubwa kama hizi huwa napendelea kuwa wa kitofauti ndiyo maana unaniona hivi.”

Leave A Reply