The House of Favourite Newspapers

Linex Kutoa ‘Yaongeze’ kwa Mashabiki Siku ya Bethidei Yake

Sunday Mangu ‘Linex’

STAA wa Bongo Fleva na mkurugenzi wa Voice Of Africa (VOA) anayetikisa na ngoma yake  ya ‘Kiherehere’, Sunday Mangu ‘Linex’ anatarajia kusheherekea siku yake ya kuzaliwa Februari 14 kwa aina yake.

Sunday Mangu ‘Linex’

Linex amefunguka kupitia mitandao ya kijamii kwamba anatarajia kuachia wimbo utakaokuwa zawadi kwa mashabiki wake. Wimbo huo utaitwa ‘Yaongeze’ na haitakuwa kwa ajili ya redio wala televisheni bali ni maalumu kwa ajili ya mtandao pekee.

Aidha amesema maandalizi ya video ya wimbo unaotikisa wa ‘Kiherehere’ yapo katika hatua za mwisho na itatoka hivi karibuni.

 

Salum Milongo/GPL

 

 

Comments are closed.