The House of Favourite Newspapers

Ditto Afunguka Kutajwa na Makonda Ishu ya Madawa

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Moyo Sukuma Damu’, Lameck Ditto amefunguka na kusema yeye hahusiki na biashara ya dawa za kulevya wala matumizi ya dawa za kulevya na kusema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikosea kutaja jina.

Ditto amefunguka na kusema kuwa hata yeye alisikia jina lake likitajwa kwenye kundi la wasanii ambao wanahitajika kufika kesho kituo cha polisi na kusema anadhani kuwa Mkuu wa Mkoa alikosea kutaja jina lake.

“Kiukweli mimi mwenyewe nimeshtuka sana maana sijihusishi kwa namna yoyote na madawa ya kulevya, siuzi wala kutumia na siku zote nayapiga vita sababu natambua si mazuri katika jamii.

“Nadhani Mheshimiwa alikosea kutaja jina maana alisema Ditto lakini baadaye niliona amerekebisha na kusema Titto, hivyo naomba Watanzania watambue mimi sihusiki na madawa ya kulevya” alisema Lameck Ditto.

Jana Februari 2, 2017, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alifanya mazungumzo na wamahabari na kueleza kuwa amedaka mtandao unaodaiwa kujihusisha na madawa ya kulevya huku akiwataja wasanii 9 na askari polisi wanaoshutumiwa kujihusisha na mtandao huo.

Miongozi mwa wasanii nao ni Wema Sepetu, T.I.D, Chid Benz, Rachel, Mr. Blue na wengine amao aliwataka wafike kituo kikuu cha polisi leo.

CREDIT: EATV

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.