The House of Favourite Newspapers

LIQUID MASTER MZEE WA GAMBE NOMA, ALAMBA MILIONI 1

Meneja Masoko wa Kampuni ya Selcom, Juma Mgori akimkabidhi hundi ya Sh milioni moja Gerald Moshi kutoka kampuni ya Moshi Shop ambaye ni mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya “Shinda Mtaji inayoratibiwa na kampuni hiyo. Droo hiyo ilichezeshwa leo jijini Dar es Salaam.

JUMLA ya wafanyabiashara sita wamejishindia mamilioni katika droo ya tatu ya promosheni ya “Shinda Mtaji inayoratibiwa na Kampuni ya Selcom na Mastercard  kwa lengo la kuwaongezea mitaji na kukuza biashara zao.

 

Promosheni hiyo iliyozinduliwa rasmi Novemba  mwaka jana inalenga wafanyabiashara wote nchini ambao wanaendelea kujiunga na kutumia huduma ya Masterpass QR katika kupokea malipo mbalimbali kwenye maeneo yao ya biashara na wafanyabiashara ambao tayari wameshajiunga na huduma hiyo.

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika makabidhiano ya hundi kwa washindi hao wa promosheni hiyo, Meneja Masoko wa Selcom, Juma Mgori alisema promosheni hiyo inamuwezesha mfanyabiashara kujishindia sh milioni moja kila wiki kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Novemba hadi Januari 2018.

Meneja Masoko wa kampuni ya Selcom, Juma Mgori akimkabidhi hundi ya Sh milioni moja Peter Nzyungu kutoka kampuni ya Irene Designing ambaye ni mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya “Shinda Mtaji inayoratibiwa na kampuni hiyo.

Alisema kila mfanyabiashara atakayejiunga na Masterpass QR na kuanza kupokea miamala kutoka kwa wateja ataingia moja kwa moja kwenye droo ya promosheni kwa wiki hiyo na kupata nafasi ya kujishidia hivyo kumuwezesha kujiongezea mtaji wa biashara yake.

 

“Masterpass QR ni huduma inayomuwezesha mteja kufanya malipo ya bidhaa na huduma mbalimbali kutoka kwenye akaunti ya simu au akaunti ya benki kwa kuingiza Pay Number ya mfanyabiashara au ku-skani kodi ya QR iliyopo kwenye eneo la mfanyabiashara kwa kutumia Smartphone.

Meneja Masoko wa kampuni ya Selcom, Juma Mgori akimkabidhi hundi ya Sh milioni moja Mmoja wa wakilishi wa baa ya Liquid, Piere Gumbo kutoka jijini Dar es Salaam ambaye ni mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya “Shinda Mtaji inayoratibiwa na kampuni.

“Kupitia huduma ya Masterpass QR, mteja ataweza kufanya malipo kupitia mitandao ya simu kutoka Tigo Pesa, M-Pesa, Airtel Money, Halopesa, Ezypesa na Selcom Card. Pia kwa upande wa huduma ya mobile banking ataweza kufanya malipo kutoka Access Bank, I&M Bank, NBC Bank, Akiba Commercial Bank, Amana Bank, BancABC, Canara Bank, Exim Bank, TPB Bank, NMB Bank, FINCA Microfinance Bank na Standard Chartered Bank” alisema.

 

Alisema wateja wa benki hizo pia wataweza kupakua Masterpass Tanzania App kupitia Smartphone na kujisajili ili kufanya malipo kwa Masterpass QR moja kwa moja kutoka kwenye akaunti zao za benki.

“Ili mfanyabiashara aweze kusajiliwa na huduma ya Masterpass QR atatakiwa kujaza fomu ya kujiunga ambayo inapatikana kwenye ofisi za Selcom, atawasilisha leseni ya biashara, hati ya TIN na kitambulisho chake na itachukua siku 2 hadi 3 kuunganishwa na huduma ya Masterpass QR,” alisema.

Aidha, alisema huduma ya Masterpass QR inalenga kuwaondolea watanzania adha ya kubeba fedha taslimu au kuwa na kadi ya benki muda wowote wanapohitaji kufanya malipo. Pia inaondoa usumbufu na gharama pamoja na kuleta usalama kwa wafanyabiashara ambao walikuwa wakikaa na fedha nyingi sehemu zao za biashara.

 

Mmoja wa washindi hao Gerald Moshi anayewakilishi kampuni ya Moshi Shop iliyopo Arusha, alitoa wito kwa wafanyabiashara kuchangamkia huduma ya Masterpass QR kwani inalenga kuwaondolea watanzania adha ya kubeba fedha taslimu au kuwa na kadi ya benki muda wowote wanapohitaji kufanya malipo.

Meneja Masoko wa kampuni ya Selcom, Juma Mgori akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya “Shinda Mtaji inayoratibiwa na kampuni hiyo. Droo hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam jana na washindi hao wamekabidhiwa hundi za thamani ya Sh milioni moja kila mmoja.

Naye Faraji Suleiman ambaye anayemiliki Faraji Hardware jijini Dar es Salaam alisema huduma hiyo ya Masterpass QR inaondoa usumbufu na gharama pamoja na kuleta usalama kwa wafanyabiashara ambao walikuwa wakikaa na fedha nyingi sehemu zao za biashara.

“Mfanyabiashara anapojiunga kutumia huduma hii fedha za mauzo ya siku zitatumwa kwenye akaunti yake ya benki au simu siku hiyo hiyo baada ya siku ya kazi kuisha,” alisema.

NA MWANDISHI WETU

Comments are closed.