The House of Favourite Newspapers

Lissu Ahojiwa Kuhusu Uchochezi wa Bombardier ya Serikali

0
Tundu Lissu akifikishwa mahakamani, picha na maktaba.
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye alikamatwa na polisi mapema leo wakati anatoka Mahakamani, amehojiwa na Polisi kwa tuhuma za kufanya makosa mawili.
Msemaji wa CHADEMA, Tumaini Makene amesema, Tundu Lissu alihojiwa na Polisi kuhusiana na makosa mawili ambayo ni;
1. Kumkashifu Rais.
2. Uchochezi kuhusu kuzuiliwa na kushikiliwa kwa Ndege ya Serikali ya Bombardier.
Tundu Lissu anadaiwa kufanya makosa hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ijumaa iliyopita, Agosti 18, 2017.
Aidha, Makene amesema, Lissu ambaye ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, amekataa kutoa maelezo yoyote Polisi, akitumia haki yake ya kisheria kuwa mtuhumiwa ana haki, kisheria, kutaja jina na anuani yake tu anapokuwa anashikiliwa na Polisi hadi atakapofikishwa Mahakamani ambako ndiko atataoa maelezo kujibu mashtaka anayotuhumiwa nayo.
Lissu amesema yuko tayari kujibu mashtaka yake Mahakamani ambapo akiwa Polisi amepata msaada wa kisheria kutoka kwa Wakili Faraji Mangula.

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Alichokizungumza Tundu Lissu Baada ya Kuachiwa na Polisi kwa Dhamana

Leave A Reply