The House of Favourite Newspapers

Lissu Asogeza Mbele Tarehe Kurejea

ALIYEKUWA Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema hatarejea Tanzania Septemba 7, 2019,  kama ilivyopangwa badala yake atasubiri ruhusa ya madaktari wanaomtibu.

Lissu ametoa kauli hiyo jana Jumanne Septemba 3, 2019,  katika mahojiano na Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC), alipoulizwa lini atarejea Tanzania.

Amesema bado madaktari hawajaweka bayana kwamba atarudi lini.

“Nilisema mwanzoni nitarudi tarehe 7 Septemba, 2019,  lakini daktari wangu ameniambia ataniona tarehe 1 Oktoba, 2019,  na mara ya mwisho ataniona mara ya mwisho tarehe 8 Oktoba, 2019, kwa hiyo ile ratiba ya mwanzo haitawezekana, kwa sababu daktari wangu anataka kuniona.” amesema.

Lissu amekuwa nje ya nchi tangu Septemba 7, 2017,  aliposhambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana akiwa eneo la makazi yake Area D, Dodoma akitoka kuhudhuria vikao vya Bunge.

Comments are closed.