The House of Favourite Newspapers

Lissu Awasili Kenya, Agoma Kufika Tanzania – Video

0

ALIYEKUWA  mbunge wa singida mashariki Tundu Lissu (CHADEMA) amesema atarejea Tanzania baada ya marafiki zake kumuhakikishia usalama wake.

 

Lissu ametoa kauli hiyo jana, Novemba 28, 2019 wakati wa mahojiano na Kituo cha Television cha KTN cha nchini Kenya baada ya kuulizwa awali hilo na mwandishi Paul Nabiso kuhusu mpango wake wakurejea nchini baada yakumaliza matibabu.

 

“Watu wenye basara lazma wakae na kuangalia namna nzuri yakufanya ili niweze kurudi nyumbani lakini nikiwa salama. Hizi jitihada zinafanywa na marafiki wa ndani na nje ya nchi kuhakikisha nakuwa salama kurudi Tanzania. Ikifika mahala wakasema usalama wangu utaangaliwa, nitarudi nyumbani.

 

“Nililetwa hapa (Nairobi) nikiwa sijitambui Wakenya walijitolea damu yao ili kuokoa maisha yangu, mimi ni Mkenya pengine sina hati ya kusafiria ya Kenya lakini nina damu ya kutosha ya Kenya ya kunifanya niwe Mkenya.

 

“Tunazungumzia mtu ambaye amepigwa risasi 16 amefanyiwa oparesheni 24 katika kipindi cha miaka miwili ni makosa kiasi gani kuuliza huyu ambaye amefanyiwa hivi na watu wasiojulikana atakuwa salama au la? Makosa kiasi gani kuuliza swali kama hilo.

 

“Nilishambuliwa Dodoma nikiwa Bungeni, spika mwenyewe alikuwepo siku ninaondolewa kuletwa Nairobi wakubwa wote walikuwepo maamuzi yalipofanyika kuletwa Nairobi sasa ni ruhusa ipi ambayo spika alihitaji katika mazingira ambayo nilikuwa sijitambui.

 

“Mimi sitaki na sijawahi kutaka kuishi uhamishoni na siko uhamishoni nilienda kwa matibabu nimeshatibiwa sasa nasubiri niambiwe usalamu wangu utakuwaje. Miaka ile ya Rais Kikwete tulikuwa tunakabiliwa na matatizo migogoro ya kisiasa na hakuna maelewano rais anatuita tunazungumza matatizo yanatataliwa

 

“Hatujawahi kukataa kukaa pamoja na serikali kuhadili mustakabali wa nchi yetu kwa masuala ya siasa isipokuwa tuna rais ambaye alitangaza hadharani kwenye TV kwamba ifikapo mwaka 2020 tunapoenda kwenye uchaguzi mkuu hakutakuwa na vyama vya upinzani.

 

“Tunakwenda kwenye maandalizi ya uchaguzi wagombea wetu wamefutwa kwa 96% nchi nzima sasa katika mazingira ya aina hii tulikuwa hatutaweza kushiriki uchaguzi wa namna hiyo. Tukienda kwenye uchaguzi mwakani, uchaguzi huru na wa haki tunaweza tukaishangaza Dunia na tukajishangaza sisi wenyewe pamoja na matatizo tuliyonayo kwa utawala huu,” amesema Lissu.

 

Kuhusu kugombea urais Tundu Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA amesema kama Chama chake na vyama vingine vya ushirika vitampa nafasi hio basi hana budi kugombea nafasi hio ya urais wa nchi.

 

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Leave A Reply