The House of Favourite Newspapers

Ripoti ya Vyombo vya Habari na Uripoti Uchaguzi Mkuu 2020 Tanzania

0

Matokeo ya Utafiti kwa namna vyombo vya Habari vya Tanzania vilivyoripoti Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2020 kwa namna vyombo hivyo vinavyofanya kazi kwenye uchaguzi huo.

 

Akisoma ripoti hiyo leo, Abdallah Katunzi, Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) amesema utafiti huo umefanyika chini ya Ubora wa Vyombo vya Habari ukiangazia uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Urais, Ubunge na Madiwani pamoja na uchaguzi wa Urais kwa upande wa Zanzibar.

 

“Asilimia 81 ya habari za uchaguzi wa mwaka 2020 zilikuwa za matukio ya uchaguzi, ni 19% tu ya habari ndizo habari ambazo vyombo vilikwenda kutafuta habari vyenyewe. Vyombo vya habari kwa asilimia kubwa vilitegemea matukio ya vyama vya siasa.

 

“Vyombo vya habari vya Serikali viliripoti matukio ya CCM kwa 41%, na matukio ya wapinzani kwa 17%. Hivi ni vyombo vinavyotakiwa fursa sawa kwa vyama vyote. Vyombo vya habari vya CCM viliripoti habari za CCM kwa 52% na 6% kwa upinzani.

 

“Vyombo vya habari binafsi viliripoti habari za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 sawa sawa (asilimia 27 kwa CCM na upinzani), hivyo vyombo hivi viliweza kusimama na kutimiza wajibu vizuri.”Gazeti la The Citizen liliripoti 7% ya habari za CCM na 40% ya habari ya vyama vyote vya upinzani. Mwananchi 20% kwa CCM na 42% kwa upinzani, Mwanahalisi 24% CCM na upinzani 46%.

“Vyombo vya habari vya Serikali viliripoti habari za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa wagombea urais kama ifuatavyo; 81% ya habari zao imeenda kwa mgombea wa CCM (Magufuli), 26% kwa Chadema (Lissu) na 11% kwa ACT-Wazalendo (Membe).

“Vyombo vya habari vya CCM viliripoti habari za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa wagombea urais kama ifuatavyo; 94% ya habari zao imeenda kwa mgombea wa CCM (Magufuli), 19% kwa Chadema (Lissu) na 07% kwa ACT-Wazalendo (Membe).

“Vyombo vya habari binafsi (ambavyo si vya Serikali wala vya CCM viliripoti habari za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa wagombea urais kama ifuatavyo; 64% ya habari zao imeenda kwa mgombea wa CCM (Magufuli), 42% kwa Chadema (Lissu).

“Upande wa Zanzibar, mgombea wa CCM alipata coverage kubwa kwenye vyombo vya habari katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Inaonekana vyombo vya habari vilivyopo Bara viliweza kuripoti kwa ulinganifu kuliko vyombo vilivyoko Zanzibar.

“Kiujumla vyombo vya habari havikuweza kuripoti Sera za vyama badala yake viliripoti yale waliokuwa wakisema wagombea tena kwa uchache. Lakini upande wa CCM ulipata coverage kubwa kuliko upande wa upinzani.

“Kuhusu vyombo vya habari kuhoji ahadi za wagombea, kati ya habari 2400, ni habari 17 tu ndizo zilizohoji ahadi za wagombea. Tafsiri yake ni kwamba ahadi zilikuwa zinatolewa na kuripotiwa kama zilivyo bila kuhoji.

“Mazingira kabla na baada ya uchaguzi hayakuwa rafiki sana kwa vyombo vya habari, Gazeti la Tanzania Daima lilifutiwa leseni siku chache kabla ya kuanza uchaguzi. Clouds FM na Clouds TV walifungiwa kwa siku 7 lakini Serikali ilitoa sababu.” Abdallah Katunzi, Mtafiti (UDSM).

 

Leave A Reply