The House of Favourite Newspapers

Kipindi cha DARASA Chatimiza Mwaka Mmoja – Video

0

KIPINDI cha Darasa kinachoruka kupitia @255GlobalRadio kimefanya hafla ya baada ya kutimiza mwaka mmoja leo Ijumaa, mei 28, 2021 tangu kuanzishwa kwake katika Ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

Kipindi hicho kina lengo la kuwafundisha wasikilizaji wake na wananchi wote kwa ujumla mbinu mbalimbali za ujasiriamali na namna ya kuendesha biashara ili wafanikiwe na kujikwamua kutoka katika wimbi la umaskini.

Hafla hiyo ambayo imeendeshwa na Watangazaji wa Kipindi hicho akiwepo mwalimu Rodrick Nabe, Mtangazaji Lukas Masungwa na wengine.

Imehudhuriwa pia na Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, walimu wa Ujasiriamali Nduku Charles Nduku, Paul Mashauri, MC Luvanda na wengine wengi Pamoja na wanafunzi wa DARASA kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Kipindi ch DARASA huruka hewani kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa 11:00 jioni.

 

 

Leave A Reply