The House of Favourite Newspapers

RC Kunenge Ahimiza Kumuaga Magufuli, Asimamisha Sherehe Zote Siku 21

0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ametoa ratiba na utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Dkt. John Magufuli ambapo kwa Mkoa huo umepewa siku mbili za kutoa heshima za mwisho.

 

 

Akitoa ratiba hiyo RC Kunenge amesema Siku ya kesho Jumamos Machi 20 kuanzia saa 1:00 -3:00 Asubuhi itafanyika Misa takatifu kanisa Katoliki Mt. Petro, Saa 3:00 – 3:30 asubuhi Mwili wa Marehemu utawasili Uwanja wa Uhuru, Saa 3:30 – 4:30 asubuhi itafanyika Misa takatifu ambapo Saa 4:30 Asubuhi adi Saa 9: 30 Alasiri Viongozi wa Serikali, Vyama vya siasa, Wafanyakazi na Taasisi za umma watatoa heshima za mwisho na majira ya saa 9:30 – 12:00 Wananchi watatoa heshima za mwisho.

 

 

Aidha RC Kunenge amesema Siku ya Jumapili Saa 2:00 Asubuhi mwili wa Marehemu utawasili Uwanja wa Uhuru, Saa 2:30 Asubuhi adi Saa 10:30 Jioni Wananchi watatoa heshima za mwisho ambapo Saa 10:30 Jioni adi Saa 11:00 jioni Mwili utaelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo saa 11:00 jioni adi Saa 11:45 jioni Mwili utasaririshwa kutoka Dar es salaam kuelekea Dodoma.

 

 

Katika hatua nyingine RC Kunenge ametoa kibali kwa Daladala, Bajaji na Bodaboda kupeleka wananchi Uwanja wa Uhuru atakama hawana route za ili kurahisisha suala la usafiri huku akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi.

 

 

Pamoja na hayo RC Kunenge amepiga marufuku kufanyika kwa sherehe kwa siku zote 21 za maombolezo.

“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza Siku 21 za maombolezo nitoe rai, nitoe agizo katika siku 21 hizo hakuna sherehe yoyote itakayoruhusiwa kufanyika sisi ni waungwana tuheshimu mila na desturi zetu za Watanzania huu ni msiba mkubwa hatuwezi kuwa na sherehe zikiendelea” amesema Kunenge.

 

 

Kunenge amewataka viongozi kwenye  mashirika na taasisi binafsi kuwaruhusu wafanyakazi wao kwenda kutoa heshima zao za mwisho kwa Hayati Dkt. Magufuli katika siku hizo mbili.

 

Leave A Reply