JPM Kufuta Sherehe za Uhuru, BAVICHA Wataka Wanachi Kwenda Magerezani – Video

Baraza Vijana la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) – BAVICHA limetoa masikitiko yake juu ya Jeshi la Polisi nchini kufuatia kukamatwa kwa viongozi wao ambao wanatumuhiwa kwa makosa tofauti ikiwemo la uchochezi.

 

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Makao makuu ya Chadema, Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Patrick Ole Sosopi amesema wanasikitishwa na jeshi la Polisi kufuatia vitendo vya uonevu ambavyo wanafanyiwa na kutaka jeshi hilo lijitathmini kwa matendo yao.

 

Kwa Upande mwingine Sosopi ametoa rai kwa wananchi kuitumia siku ya maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika, Desemba 9, 2018 kuwatembelea wafungwa walioko katika magereza mbalimbali huku akipinga agizo la Rais John Magufuli la kufutwa kwa sherehe za Uhuru na fedha hizo kutumika kujengea Hospitali mkoani Dodoma.

 

Sosopi amewataka wananchi siku hiyo kutii sheria za magereza na kuwaeleza wafungwa na mahabusu wa makosa mbalimbali kwenye magereza hayo kuhusu hali ya maisha ilivyo uraiani akidai kuwa hakuna uhuru kama ilivyo kwa waliyoko magerezani.

 

VIDEO: MSIKIE SOSOPI AKIFUNGUKA

Toa comment