The House of Favourite Newspapers

BOT YAHAMISHA MALI, MADENI YA BANK M KWENDA AZANIA BANK- VIDEO

BENKI Kuu nchini (BoT)  imeamua kuhamisha, kwa mujibu wa sheria, mali na madeni ya Bank M kwenda Azania Bank Ltd.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, wateja wenye amana na wadai wengine wa Bank M wataarifiwa ni lini watapata huduma kupitia Azania Bank na wale wenye mikopo wanatakiwa kuendelea kulipa mikopo yao kulingana na mikataba yao, na Benki Kuu italisimamia hilo kwa karibu.

 

Mtaji wa Azania unatajwa kufikia kiasi Shilingi za Tanzania bil 164,  kiwango ambacho ni cha juu zaidi kwani mtaji unaotakiwa kisheria ni Sh. bilioni 15.

 

Benki Kuu imesema itaendelea kuwalinda wateja wenye amana nchini ili kuimarisha sekta ya benki nchini.

 

Wakati huohuo BoT imesema watu wenye hisa na  wadaiwa wa Bank M, wafike katika benki hiyo (BoT) ndani ya siku saba ili kufikia makubaliano kutokana na hali hiyo iliyopo sasa.

 

 

Comments are closed.