The House of Favourite Newspapers

LIVE: Hatimaye Yanga Warejea Nyumbani Wakitokea Algeria

0

   Klabu ya Yanga wamerejea nyumbani wakitokea nchini Algeria walikokuwa wamekwenda kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika ambapo wameondolewa baada ya kufungwa na Mc Alger bao 4-0 Jumamosi.

Baadhi ya wachezaji wa Yanga walikwama kurejea nyumbani baada kuchelewa usafiri wa ndege juzi. Kaa karibu na GLOBAL TV ONLINE, inakuletea mapokezi ya Yanga LIVE.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema haya;

“Tunamshukuru Mungu tumerudi salama, kilichotokea mpaka tukachelewa ndege ni kutokana na eskoti ya polisi kuwachelewesha kwani eskoti za kule zina limit speed na huwa hazina utaratibu wa kuvuka kwenye mataa hovyo kama za huku zikifika zinasuburi foleni na siku hyo kulikua na foleni sana ndio chanzo kikubwa cha kuchelewa kwetu”, Alisema Mkwasa.

Leave A Reply