The House of Favourite Newspapers

JPM: Wanaosema Vyuma Vimekaza, Waweke Grisi la Sivyo Vitavunjika (Video)

RAIS John Magufuli amesema kuwa wanaodai maisha ni magumu mitaani huku wakitumia msemo wa “vyuma vimekaza”, basi waviwekee grisi vilainike, vinginevyo vitavunjika kabisa. Amesema hayo leo Alhamisi Desemba 14,2017 alipofungua mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

Rais ameyasema hayo leo Desemba 14, 2017 mjini Dodoma wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ambapo amesema waliokuwa wanapata fedha kwa njia zisizo halali ndiyo wanaosema vyuma vimekaza, wqanaojishughulisha wanapata pesa zao halali na maisha wanayamudu vizuri.

“Wanaosema vyuma vimekaza na bado, vitavunjika kabisa, labda waweke grisi,” amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amesema wakati anaingia madarakani alikuta changamoto nyingi zikiwemo za wafanyakazi hewa, vyeti feki, wizi na ufisadi ambapo baada ya kufanya jitihada za dhati za kudhibiti, watumishi wa umma 12,000 wamepatikana na vyeti feki wakiwemo walimu 3,655 tangu walipoanza kuhakiki huku uhakiki huo ukibaini watumishi hewa 20,000 na kwamba, Serikali ilikuwa inapoteza fedha nyingi kuwalipa mishahara hewa.

“Kila kitu kilikuwa hewa, watumishi hewa, pembejeo hewa, TASAF hewa, hata mapenzi inawezekana yalikuwa hewa. Kutokana na udhibiti wa fedha za Serikali ni lazima watu waliokuwa wanapata fedha kwa njia zisizo halali watalalamika kuwa vyuma vimekaza,” alisema JPM.

Kuhusu madai ya walimu, amesema Sh25 bilioni wanazoidai Serikali zitalipwa baada ya uhakiki kumalizika” amesema Rais Magufuli.

 

Comments are closed.