The House of Favourite Newspapers

Magufuli: Nililala Nyumbani kwa Mzee Sitta – Video

0

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),  John Magufuli, aameendelea na kapmbeni zake katika viwanja vya Mirambo, wilayani Urambo mkoani Tabora, kuinadi Ilani ya CCM ya 2020-2025 kisha kuomba kura wananchi wa mkoa huo leo Septemba 21, 2020.

 

Akiwahutubia wananchi wa Urambo, Magufuli amesema:

“Miaka mitano iliyopita nilikuja Urambo hapakuwa na watu wengi namna hii, Urambo mmefunika, Urambo oyee! Sikutegemea hata barabara za lami zingekuwa nyingi namna hii hapa, kila kona lami, najua zinahitajika nyingine, mchagueni Margaret Sitta aongoze njia.

“Nilipokuja hapa Urambo nikamkuta huyu Mgogo ametoka Makao Makuu Dodoma mpaka hapa, hii inadhihirisha urafiki uliyokuwepo kati ya Chifu Mirambo na Chifu Mazengo enzi zile, Mheshimia Ndugai amekuja kwao, na kaupara kake kama mtoto wangu wa kwanza aliyepotelea Dodoma.

 

“Nakumbuka wakati nikiwa Waziri wa Ujenzi Mzee Sitta akiambatana na mke wake Margaret, bahati nzuri Margaret tumesoma naye Chuo Kikuu, nikajiuliza huyu mzee amekuwa waziri tangu nasoma sekondari, amefuata nini, nikamsikiliza.

 

“Mzee Sitta akanipa historia ya Urambo na Tabora kupigania Uhuru, wakoloni hawawezi kutoa pesa za kujenga barabara kwa sababu wanafahamu misimamo ya watu wa Tabora tangu enzi za ukoloni, akaniambia naomba ufanye mikakati yote tupate barabara ya lami.

 

“Nikapeleka hilo ombi Serikalini likapita na fedha zikatengwa, tukaanza kupasua barabara za Tabora. Wakati nakuja kuweka jiwe la msingi nililala kwa Mzee Sitta wakati huo akiwa Spika, pakiwepo na mama yake namkumbuka, mzee akaniambia umetengeneza ya kupita huko, tengeneza na ya kupita mjini.

 

 “Nafahamu kuna changamoto ya maji hapa Urambo mjini licha ya kuchimba visima kumi, ukishapata mke ni rahisi kupata watoto, tulianza kupeleka maji Tabora mjini, na Mama Sitta alinifuata Ikulu akaniomba, sasa tunayaleta hapa, wanawake wazuri wasioge matope waoge maji.

 

“Mradi ukishamalizika Urambo tutaupeleka na Kaliua, nina uhakika hawatafanya makosa kama walivyofanya miaka mitano iliyopota, wakifanya makosa tena shauri yao,” amesema Magufuli.

 

Leave A Reply