The House of Favourite Newspapers

Kamanda Sirro: Waendesha Bodaboda Mwisho Saa 6 Usiku

RPC wa Kinondoni, Suzan Kaganda akizungumza.

Kamanda Sirro akizungumza na wakazi wa Ally Maua, Kata ya Kijitonyama, Dar.

Mkazi wa Ally Maua akiuliza swali kwa Kamanda Sirro.

KAMANDA Mkuu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema kuwa kuanzia sasa, wote wanaofanya biashara ya kusafirisha abiria kwa njia ya pikipiki maarufu kama bodaboda mwisho saa 6 usiku kwa Jiji la Dar.

Sirro ameyasema hayo leo wakati alipofanya mkutano na wakazi wa Mtaa wa Ally Maua, Kata ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

“Unakuta mtu anafanya biashara kuanzia asubuhi mpaka jioni, na usiku napo anataka akeshe… wewe ni mtu gani? Hao wanaojifanya wanabeba abiria usiku kumbe ndiyo wezi… hiyo hatukubali… sasa kuanzia sasa, mwisho wa bodaboda kufanya kazi ni saa 6 usiku, ukikamatwa zaidi ya saa 6 utalala kituo cha polisi, ” alisema Kamanda Sirro.

Kuhusu madawa ya kulevya Kamanda Sirro amesema kuwa jeshi lake linaendelea na oparesheni ya kuwasaka wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya, bangi pamoja na pmombe haramu ya gongo.

Pia ameongeza kwamba jeshi hilo halimuonei mtu bali linafanya kazi yake kwa kufuata sheria na endapo mtuhumiwa akikamatwa kwa matumizi ya dawa za kulevya anapelekwa kwa mkemia kupimwa kabla ya kuchukuliwa hatua.

Aidha Kamanda Sirro amewaonya wale wanaozifanya nyumba za ibada (makanisa na misikiti) kuwa za kutolea mafunzo ya judo, karate na kung-fu badala ya kutangaza neno la Mungu waache tabia hiyo mara moja kwani jeshi lake limejipanga kuwakabili kwa namna zote.

PICHA ZOTE NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

 

Wakatia Kamanda Sirro akizungumza hayo, Global TV Online ilikuwa LIVE na haya ndiyo aliyoyasema… Bofya PLAY utazame VIDEO yote.

Comments are closed.