The House of Favourite Newspapers

RIPOTI YA MCHANGA II: Alichokisema Rais Magufuli Baada ya Kukabidhiwa, INASIKITISHA!

0

IKULU, DAR: Ripoti ya pili ya mchanga wa madini, imewasilishwa mbele ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mwenyekiti wa kamati hiyo, Prof. Nehemia Eliachim Ossoro ambapo rais ameonesha kuhuzunishwa na kukasirishwa na kilichomo kwenye ripoti hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika Job Ndugai, Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim wakiwa katika picha na kamati ya Rais ya pili ya kuchunguza makinikia na mustakabali wa sekta ya madini nchini baada ya kupokea ripoti yao Ikulu Dar es salaam leo.

Ripoti ya kamati hiyo, inakuja siku chache baada ya kamati ya kwanza iliyoongozwa na Profesa Mruma, nayo kukabidhiwa kwa mheshimiwa Rais, ikionesha ubadhirifu mkubwa wa rasilimali za taifa, katika sekta ya madini nchini.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika Job Ndugai, Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim wakiwa katika picha na kamati ya Rais ya pili ya kuchunguza makinikia na mustakabali wa sekta ya madini nchini na vingozi wa vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya kupokea ripoti yao Ikulu Dar es salaam leo.

Akisoma ripoti hiyo mbele ya Rais Magufuli, Prof. Ossoro amesema;

Kamati yake imebainisha kuwa kupitia hati ya usafirishaji wa melini, idadi kubwa ya makontena yalikuwa yakisafirishwa bila kuorodheshwa.

Idadi na uzito wa makontena ya mchanga ulionekana kuwa mkubwa kwenye meli tofauti na kwenye nyaraka za bandarini.
Bulyanhulu na Pangea wamekuwa wakiuza makinikia nje ya nchi kinyume na taratibu.

Wamedanganya uzito wa makontena yao.
Kamati imebaini kuwa Acacia Mining PLC inafanyakazi za uchimbaji wa madini nchini kinyume na sheria.

Makontena 30 ya futi 20 yenye makinikia yalionekana kwenye nyaraka yamesafirishwa, lakini ukweli yalisafirishwa 33.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika Job Ndugai, Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim wakiwa katika picha na kamati ya Rais ya pili ya kuchunguza makinikia na mustakabali wa sekta ya madini nchini na vingozi wa vikosi vya Ulinzi na Usalama na baadhi ya wanahabari baada ya kupokea ripoti yao Ikulu Dar es salaam leo.

Viwango vya dhahabu kwa kila kontena ni 28kg, kwa miaka yote ni tani 1,240 kwa kiwango cha chini, thamani yake Tsh 108 trilioni
Katika hafla iliyofanyika ikulu na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, wa kisiasa, kidini na kijamii,

Rais Magufuli amezungumza kwa uchungu kuhusu ripoti hiyo, na jinsi Watanzania wanavyoendelea kuteseka kwa umaskini wakati rasilimali zao zikisafirishwa nje ya nchi kwa njia zisizo halali.

Aidha kamati hiyo imetoa mapendekezo 20 ikiwa ni pamoja na;

1. Serikali kupitia msajili wa makampuni iichukulie hatua kampuni ya Acacia kwa kufanyakazi kinyume na sheria.

2. Serikali izuie usafirishaji wa makinikia nje ya nchi, hadi hapo wadaiwa watakapolipa madeni yao.

3. Serikali iwachukulie hatua waliokuwa Mawaziri, Wanasheria Wakuu wa Serikali, Manaibu na watumishi wote waliohusika.

4. Serikali ijenge smelter hapa nchini ili kuokoa fedha zinazopotea kutokana na usafirishaji wa makinikia.

5. Serikali ichunguze mwenendo wa watumishi wa Mabaraza ya Kodi kwa kuchukua muda mrefu kutoa maamuzi ya mashauri ya kodi.

6. Sheria iongoze kiwango cha adhabu kilichoanishwa katika ukiukwaji wa sheria ya madini nchini.

Kuhusu sakata la kampuni ya Acacia, mheshimiwa rais amesema ameshangazwa sana na ripoti kwamba kampuni hiyo haikuwa imesajiliwa nchini na msajili wa makampuni, Brela wala haikuwa ikilipa kodi kama inavyostahili, licha ya kusafirisha kiwango kikubwa cha dhahabu na mchanga wa dhahabu.

Aidha Rais Magufuli ameyapokea mapendekezo yote 20 ya kamati ya pili ya madini na kuvitaka vyombo vya usalama viwahoji wahusika wote waliotajwa.

Rais pia amesema amesema iwapo Accacia inahitaji kuendelea kufanya biashara Tanzani, lazima ilipe pesa zote ilizoiibia nchi ndipo isajiliwe huku akimuagiza waziri wa sheria kuunda timu ya wanasheria wazalendo, waunde sheria zipelekwe bungeni ili zikafanyiwe marekebisho pamoja sheria zote za gesi na za madini zipitiwe upya, zikafanyiwe marekebisho kuondoa mapungufu yanaoleta mianya ya wizi.

Leave A Reply