The House of Favourite Newspapers

Video: Kheri James Amchana Waziri Katambi – “Mabando Bado Yapo Juu”

0

Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umeitaka Serikali kuingilia kati suala la gharama zinazotozwa katika vifurushi vya huduma za mawasiliano.

 

Mwenyekiti wa UVCCM, Kheri James ametoa kauli hiyo leo Jumapili Mei 23, 2021 alipokuwa akizungumza kwenye Baraza kuu la umoja huo, ambapo amesema vijana wamekosa ajira na wanaishi maisha magumu kutokana na kupanda kwa gharama za vifurushi.

“Tunaona namna lugha inavyogongana kuhusu masuala ya bando,leo mnasema hivi kesho mnasema vile,keshokutwa mnabadilisha hivi. Haya mambo sisi hatuyakubali,” amesema James

 

Amesema vijana wengi wamejiajiri kwenye mitandao ya kijamii inayohitaji vifurushi na kwa sasa ajira hiyo imeshuka kwa kasi kubwa kutokana na gharama kubwa za vifurushi.

 

James ameitaka Serikali Kuangalia namna bora ya kuliweka sawa jambo hilo na kuleta afueni kwa wananchi kwakuwa vifurushi sio kwa ajili ya kuangalia sinema ni sehemu ya ajira.

 

“Hizi Mbs zinatumika kufanya biashara siku hizi.Wale vijana ambao ajira zao tumeshindwa kuwapa huko kwingine, wameamua kujiajiri kupitia hapa,” James

 

Amesema kwa dunia ya sasa biashara, kazi, masomo vyote vimehamia mtandaoni hivyo kupanda kwa gharama kumeathiri watumiaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) iliyoajiri watu wa kada tofauti.

 

Naye Naibu Waziri wa nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, kazi, vijana na ajira, Patrobas Katambi amesema zaidi ya vijana 7000 waliomaliza vyuo vikuu mwaka 2019/20 wamepewa fursa mbalimbali ikiwemo kupelekwa masomo ya vitendo (internship) katika maeneno mbalimbali kujifunza.

Katambi amesema kuna vijana 136 walienda nchini Israeli kupata mafunzo ya uchumi wa kijani na hivi sasa Serikali inawatengenezea mazingira mazuri ya kukitekeleza walichojifunza.

Katambi ametoa wito kwa UVCCM na wananchi kushikamana na kulisaidia Taifa.

Amesema anatambua kuna changamoto nyingi ambazo vijana wanazipitia na mara nyingi zimesababisha chuki baina yao.

“Naomba tupunguze mioyo ya nongwa na chuki, tupendane ili tuungane na tufikie malengo. Isifike sehemu ukaanza kusema ‘unajua mimi yule katibu wetu simpendi tu’ ukiulizwa kwa nini unasema damu yangu haipatani, ukiulizwa lini amekuongeza damu hupati majibu,” Katambi

 

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply