The House of Favourite Newspapers

MAZISHI YA MAMA ABDUL: Mwili Ulivyowasili Nyumbani, Joti, Mc Pilipili Huzuni! – VIDEO

Mwili wa Muigizaji Mkongwe, Salome Nonge maarufu kama Mama Abdul, unatarajia kuzikwa leo katika makaburi ya Chang’0mbe Maduka Mawili jijini Dar, leo Januari 28, 2019.

Kabla ya mazishi mwili huo umewasilishwa nyumbani kwake Mburahati ambapo ndipo msiba ulipo na kufanyiwa ibada na baada ya hapo utawasilishwa kanisani na mapema baadaye saa saba kamili mchana utapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

Mama Abdul alifariki dunia juzi Januari 25, akiwa nyumbani kwake na inasemekana kuwa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la homa ya ini.

Kabla ya Umauti kumfika Mama Abdul alikuwa akiigiza tamhiliya ya ‘Mwantumu’ inayorushwa na DSTV ambayo ndani yake ameshirikiana na Joti, lakini pia aliwahi kunga’ra kwenye filamu kama Kantangaze.

“‘Ina Liilah Waina Lillah Rajuun”

 

 

 

 

Comments are closed.