The House of Favourite Newspapers

FULL TIME: MAJIMAJI 1-1 YANGA KUTOKA UWANJA WA MAJIMAJI

0

 

Kikosi cha timu ya Yanga Kilichoanza dhidi ya Majimaji leo katika Uwanja wa Majimaji Songea.

 

MPIRA UMEKWISHAAAAAA DAKIKA 4 ZA NYONGEZA

DK 90, Yanga wanapiga krosi nyingine safi kupitia Daud lakini inakuwa kubwa
Dk 89 krosi safi ya Kessy, kidogo tu Ngoma anachelewa kuuwahi mpira

Dk 88, Kidogo inaonekana Majimaji wana hofu sana wakipoteza mipira mingi zaidi pale katikati
SUB Dk 86 Said Juma Makapu anaingia kuchukua nafasi ya Martin ambaye ametoka baada ya kupigwa kiwiko

Dk 83, Kuna mchezaji wa Yanga ameumia, yuko chini pale wanajaribu kumpa oxygen, ni Emmanuel Martin, alipigwa kiwiko na Salamba

Kikosi cha timu ya Majimaji.

Dk 82, Yanga wanafanya shambulizi jingine kali hapa lakini shuti la kesi linapaaa juuu

GOOOOOOOO Dk 79, Krosi saaafi, Ngoma anaruka mbele ya Tumba Sued na kuandika bao la kusawazisha kwa Yanga.

Dk 78, Yanga wanapata kona ya sita, inchongwa Majimaji wanaokoa na kuwa kona tena, inachongwa tena, Humud anaokoa hapa
Dk 76, Dante anafanya kazi ya ziada hapa kumdhibiti Tegete
Dk 73, presha ya mchezo inazidi kuwa kubwa zaidi na Yanga ndiyo walioongeza mashambulizi zaidi huku Majimaji wakifanya mashambulizi ya kushitukiza
Dk 70, Yanga wanafanya shambulizi kali, Chirwa anaingia vizuri lakini krosi yake inaokolewa na Salamba

SUB Dk 66 Hassan Kessy anaingia kuchukua nafasi ya Juma Abdul.
Dk 65, mpira unaonekana kuwa na presha zaidi kwa kuwa Yanga wanataka kusawazisha na Majimaji wanalinda zaidi.
Dk 62, Juma Abdul yuko chini akitibiwa baada ya kugongwa usoni na Mapunda.

Dk 60, Mapunda anaingia na kuachia mkwaju mwingine lakini unapita juu ya lango la Yanga
Dk 59, Ntala anafanya kosa kwa kupangua mpira unaotua kwa Tshishimbi lakini shuti lake linapaa

Dk 58, Selembe anamtoka Juma Abdul na kuachia krosi kali lakini inatua mkononi mwa Selembe.

Dk 56 sasa, mpira unaonekana umechangamka kidogo ingawa Majimaji wanaoneana kuzidi kujiamini.

GOOOOOOO Dk 53, Peter Mapunda anaachia mkwaju mkali sana kutoka kushoto ya uwanja baada ya kupokea pasi safi ya Kaheza na kuandika bao.

Dk 50, Dante anafanya kazi ya ziada kuondosha mpira langoni mwake.
Dk 46 Yanga wanaonekana wameanza kwa kazi na krosi safi ya Juma Abdul inaokolewa.
Dk 45, Abdulhalim Humud anaingia kuongeza nguvu upande wa Majimaji.

MAPUMZIKO
Dk 45 + 2, Salamba analala na kuokoa mpira baada ya kuwa ametokwa na Ajibu.

DAKIKA TATU ZA NYONGEZA
Dk 45 Rostande analazimika kutoka langoni na kuokoa mpira.
Dk 44, bado hakuna bao na hakuna mashambulizi makali sana zaidi ya yale ya rasharasha.
Dk 41, Kibiga anaachia shuti safi la juujuu lakini inakuwa goalkick.
Dk 40, kona safi ya Kaheza, Tumba anajitwika lakini mwamuzi anasema alishacheza faulo kumsukuma Dante.
Dk 39, Tshishimbi anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa Selembe  na kuwa kona ya Majimaji.
Dk 36, Yanga wanapata kona inachongwa, Majimaji wanaokoa. Daud anairudisha Kaheza anaokoa tena.
Dk 33, krosi safi ya Juma Abdul lakini Ntala analazimika kufanya kazi ya ziada kuokoa.

Dk 31, Ngoma anapata nafasi ya kushuti lakini anaachia shuti nyanya na kipa Ntala anadaka kwa ulaini kabisa.
Dk 31, Hassan Juma anaruka juu na kuondosha mpira wa adhabu wa Ajibu
Dk 27, Mwashiuya anaingia vizuri lakini Juma anaokoa na kuwa kona ya tatu ya Yanga, inachongwa wanaokoa
Dk 26, Rostande ameamka, Majimaji wanachonga kona safi hapa, Tumba anapiga kichwa na kuwa goalkick
Dk 24, kipa Rostande wa Yanga anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa Mapunda uliokuwa unajaa wavuni na kuwa kona, ila Mcameroon huyo yuko chini inaonekana kaumia
Dk 22, Dante anaokoa, Majimaji wanapata kona, inaokolewa vizuri na Raphael Daud
Dk 21 sasa, mpira zaidi unachezwa katikati lakini bado hakuna timu inaweka sana mpira chini kutokana na ubovu wa uwanja

Dk 18, Mpoki anamkwapua Juma Abdul na sasa yuko chini, alikuwa akijaribu kumpita lakini bahati mbaya akamgonga mguu
Dk 16, Salamba anafanya kazi ya ziada kuondosha hatari langoni mwake wakati Chirwa akivizia, inakuwa kona. Yanga wanachonga kona safi, inaokolewa
Dk 14, Juma Abdul anachelewa  kuokoa, Mrwanda anaingia lakini Tshishimbi anaokoa vizuri hapa
Dk 12, Yanga wanachonga kona safi hapa lakini Majimaji wanaokoa vizuri kabisa

Dk 10, Mwashiuya anawatoka mabeki Majimaji lakini Kennedy anaokoa na sasa yuko chini pale, kona
Dk 7, Kaheza naye anaonyesha anataka kuipasua ngome ya Yanga lakini wako makini

Dk 4, MWashiuya anajaribu kuingia tena lakini Majimaji wanaondosha
Dk 1, mechi inaanza kwa kasi na Yanga wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Majimaji, lakini Tumba Sued anaondosha.
Leave A Reply