The House of Favourite Newspapers

Mvua Yasababisha Mafuriko Makubwa Dar, Mmoja Afariki Dunia (Picha +Video)

Tazama video kujionea hali halisi ilivyokuwa

MVUA zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimesababisha mafuriko makubwa katika Bonde la Mto Msimbazi, maeneo ya Daraja la Kigogo Wilaya ya Ilala, Jangwani, Vingunguti na maeneo mengine ambayo Mto Msimbazi unapita.


Mpaka sasa, mtu mmoja ameripotiwa kupoteza maisha eneo la Jangwani. Aliyefariki ametambulika kwa jina moja la Imma na inaelezwa kwamba alikuwa akijishughulisha na kazi ya kuokota chupa tupu za plastiki.

 

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, linaendelea na kazi yake ya uokoaji na bado maji yanaendelea kuja kwa kasi kutokea maeneo mbaimbali yaliyopata mvua kubwa kuanzia majira ya usiku.

Wananchi wengi ambao nyumba zao zimeingiwa na mafuriko, wanahaha wakiwa hawajui nini itakuwa hatima yao, kutokana na nyumba zao kuingiwa na maji ambayo yameharibu na kusomba vyombo vya ndani, yakiwemo magodoro, vitanda na vyombo vya jikoni.

 

 

 

 

 

Picha na GABRIEL NG`OSHA/GPL
 

Comments are closed.