The House of Favourite Newspapers

Mwana: Tuungane Kuukabili ‘Unga’

Mwanaheri

WAKATI Taifa likiwa katika vita dhidi ya matumizi, usambazaji na usafi rishaji wa madawa ya kulevya ‘unga’, muigizaji wa filamu Bongo, Mwanaheri Ahmed ‘Mwana’ amewataka mastaa wote kuungana pamoja ili kulikabili janga hilo la kitaifa.

Mwanaheri

Akiteta na Za Motomoto News , Mwanaheri alisema tasnia ya filamu imejikuta ikipoa kwa muda kutokana na baadhi yao kutajwa katika tuhuma za madawa ya kulevya, hivyo sasa ni muda wa mastaa wote kupiga vita madawa ya kulevya kwani yanarudisha nyuma maendeleo pia yanapoteza nguvu kazi ya taifa ambayo ni vijana.

“Madawa ya kulevya yanaathiri taifa zima, hivyo ombi langu kwa mastaa ni kwamba tuungane kwa pamoja kupiga vita maana tuna nguvu kubwa katika jamii inayotuzunguka hivyo tutumie nguvu hiyo kuyatokomeza,” alisema.

Comments are closed.