The House of Favourite Newspapers

LIVE: Mama Samia Suluhu Ahamia Dodoma Rasmi

MAKAMIU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan, leo Ijumaa, Desemba 15 amehamia rasmi makao makuu ya nchi Mjini Dodoma ikiwa ni utekelezaji wa dhamira na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhamia mkoani humo.

Samia baada ya kuwasili nyumbani kwake Kilimani Mjini Dodoma, Samia ameomba wananchi wa mkoa huo kuonyesha ushirikiano katika kufanya kazi ili kulisukuma gurudumu la maendeleo na kutimiza adhima ya serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.

 

“Nimekuwa hapa Dodoma kwa muda mrefu kidogo kama wiki moja, lakini nilipangiwa kuhamia rasmi leo Desemba 15. Hakika nimefurahi sana kwamba nitafanya kazi sehemu yangu ya kazi ya kudumu. Kauli mbiu yangu ya kwanza kwa wakazi wa Dodoma ni kuufanya mji huu kuwa wa kijani, Desemba 21 nitaendesha mpango wa kupanda miti katika wilaya zote. Kwa kuwa nasimamia pia masuala ya mazingira nitaendesha zoezi hilo ili kurudisha hali ya Dodoma,” amesema Samia.

VIDEO YA SAMIA SULUHU AKIHAMIA DODOMA

Comments are closed.