The House of Favourite Newspapers

LIVE: Makomando Wakikinukisha Maadhimisho ya 56 ya Uhuru wa Tanzania

Leo, Disemba 09, 2017 Tanzania inaadhimisha miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) ambapo sherehe hizo zinafanyika katika Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.

Katika Maadhimisho hayo ya Uhuru wa Tanzania Bara, Rais Dkt. ndiye Mgeni Rasmi. Viongozi wengi wameshawasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya kujumuika na Watanzania wengine kusherehekea.

Kikosi cha Jeshi la Wananchi Tanzani (JWTZ) na vikosi vingine vya ulinzi wanapita mbele ya Rais na Amri jeshi Mkuu kutoa salam zao za heshima kwa mkuu huyo wa nchi.

Sherehe hizi zinaadhimishwa huku kukiwa na simanzi kitaifa kufuatia askari wetu wanaolinda amani DRC kuuawa na wengine kujeruhiwa vibaya kufuatia shambulizi lililofanywa na waasi.

LIVE: Makeke ya JWTZ Maadhimisho ya Miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania

Comments are closed.