The House of Favourite Newspapers

Mobeto, Dullvan, Barnaba Wateuliwa Kuwa Mabalozi – VIDEO

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewateua Mwanamitindo Maarufu Bongo, Hamisa Mobeto, Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barnaba pamoja na Mchekeshaji maarufu, Dullvan, kuwa Mabalozi wa kuhamasisha Matumizi mazuri ya Mitandao ya kijamii ili jamii iweze kuelimika juu ya namna ya kuitumia mitandao kwenye kujiletea Maendeleo binafsi na Taifa zima kwa ujumla.

 

Wakizungumza katika hafla ya kuzindua Kampeni ya ‘Be Smart’ inalolenga kutokomeza kabisa matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, Mobeto, Barnaba na Dullvan wamesema umefika wakati sasa jamii inalazimika kubadilika na kuachana na tabia ya kuitumia mitandao kwa ajili ya kutukana watu, kusambaza picha za utupu au zisizo na maadili, badala yake waitumie kutangaza biashara zao.

 

FUATILIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.