The House of Favourite Newspapers

JPM Atoa Siku 60 Kwa Mashirika na Taasisi Yasiyotoa Gawio – Video


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Novemba 24, 2019 amepokea gawio, michango na ziada ya Serikali kutoka mashirika, kampuni na taasisi mbalimbali ambazo zinamilikiwa na Serikali.

Hafla ya kupokea gawio, michango na ziada hiyo inafanyika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Akiongea katika hafla hiyo amesema haya ”Tuna mashirika na taasisi mbalimbali 266 mpaka leo ambayo yamechangia gawio kwa Serikali ni 79, nawapongeza sana mliochangia zaidi ya Tilioni 1 kwa ajili ya manufaa ya taifa hili.

”Lakini tujiulize katika mashirika hayo 266 yaliyochangia ni 79 Serikali imeweka mtaji wa Tilioni 59.6 ukitoa 79 yanabaki mashirika 187 haya mashirika hayana habari ya kuchangia yana bodi na bodi zenyewe zina wenyeviti wanalipana posho kila wanapokaa, zina machifu executive ambao wanapanga semina na mikutano mbalimbali na wanasafiri, wanastarehe wanamagari.
“Hatuwezi kuendelea kukaa na mashirika ya namna hii, Waziri wa Fedha natoa siku 60 kuanzia leo, wawe wameshakabidhi kwako gawio, wasipo kabidhi kwako gawio bodi zile zijivunje zenyewe”

”Yapo mashirika ambayo mishahara yao inalipwa na Serikali wamepewa nyumba wengine sasa ndugu zangu mnaweza kujiuliza ungekuwa wewe ndo Rais ungefanyaje tena unaweza kukuta wengine wamelala kwenye hoteli wanatuangalia kwenye TV”  ameyasema Rais Magufuli

Comments are closed.