Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaapisha Mawaziri na Manaibu Mawaziri wapya walioteuliwa kufuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika Oktoba 7 mwaka huu.
Hafla hiyo ya uapishaji inafanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam na imehudhuriwa na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali, Bunge na Mahakama.