The House of Favourite Newspapers

Magufuli Kuchangia Mil. 400 Ujenzi Kituo cha Afya Moro – Video

Rais Magufuli

RAIS John Magufuli leo Alhamisi Julai 25, 2019,  ameahidi kutoa Sh. mil. 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha Kisaki kilichopo mkoani Morogoro huku akiwataka wakazi wa eneo hilo kuchapa kazi za kujiletea maendeleo.

 

Magufuli ametoa ahadi wakati akizungumza na wananchi eneo hilo lililopo katika halmashauri ya Morogoro vijijini ambako alitoa agizo kwa mawaziri wake, Ummy Mwalimu (Afya) na Seleman Jafo wa Tamisemi kuhakikisha wanasimamia ujenzi huo haraka.

 

Kiongozi huyo mkuu wa nchi alikuwa safarini kwenda Rufiji kwa ajili ya kuweka jiwe na msingi la mradi wa kufua umeme wa megawati 2,115 wa Stigler’s  Gorge uliopo mikoa ya Pwani na Morogoro.

 

Magufuli  alifikia uamuzi huo, baada ya wakazi hao kumweleza hawana kituo cha afya katika eneo hilo.

“Kwa nini hakuna kituo cha afya na kuna watu wengi hapa? Nataka kituo cha afya kianze kujengwa mara moja; nitamuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) ashughulikie.

“Nawapa siku saba,  tafuteni eneo, tujenge hospitali ambayo imejengwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.  John Magufuli,” alisema.

Comments are closed.