The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Awataka Waandishi Kuzingatia Mila, Desturi za Kiafrika Kuandika Mazuri -Video

0
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka waandishi wa habari kuandika habari kwa kutunza na kuheshimu mila na desturi za kiafrika.

 

Akuzungumza leo Jumanne Mei 3, 2022 katika maadhimisho ya Siku ya Vyombo vya Habari Duniani ambayo kitaifa imefanyikia jijini Arusha, Rais Samia amesema kukopa mila na desturi husababisha migongano isiyo ya lazima.

 

“Uhuru wa habari hauchagui mipaka hivyo pamoja na hilo waandishi wa habari wanatakiwa kuzingatia mila na desturi za kiafrika kuandika mazuri ikiwemo vivutio vyote vilivyomo,” amesema Rais.

Amesema ni vyema wakaandika habari ka kuthamini rasilimali zilizopo Afrika ni vyema kujivunia rasilimali mlizonazo pamoja na kuzilinda.

 

“Lakini nawaambieni tu kikubwa ni utashi wa kisiasa kwa sababu baada ya Uhuru wa Tanganyika nchi yetu ilikuwa na magazeti 10 kwa sasa ni 285, Kituo cha Redio kimoja kwa sasa ni zaidi ya 200, hatukuwa na Televisheni, blogu wala Majukwaa ya Mtandaoni

 

Tanzania ina sifa ya kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari na pengine nchi zingine walipenda kuja kuona ni kwanini tumepiga hatua kiasi hiki ndio maana waliamua siku hii ifanyikie Tanzania

 

Kanuni na Taratibu zetu ndizo zinazoruhusu uanzishwaji wa vyombo hivi na bila shaka wingi wa vyombo vya habari unaongeza uhuru wa kujieleza na uhuru wa kusambaza habari

 

Ni ukweli kwamba kuongezeka kwa idadi ya vyombo vya habari umechangiwa na sehemu kubwa ya kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano lakini ni ukweli usiopingika kuwa utashi wa kisiasa, maelekezo ya kisheria

 

Hatuwezi kukataa kuwa mitandao ya kijamii imekuwa na umuhimu katika maisha yetu, inatuo fursa ya kutumia uhuru wetu wa kujieleza jinsi tunavyoweza

 

Ukinikuna vizuri mimi nitakukuna na kukupapasa huku nakupuliza ufuuuuuu, lakini ukinipara nitakuparura, twende tufanye kazi kwa uungwana, twende tufanye kazi kwa kuelewana..sheria ziko pale pale” amesema Rais Samia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Mei 3, 2022 anashiriki maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani ambapo kwa Afrika yanafanyika Tanzania jijini Arusha.

Leave A Reply