The House of Favourite Newspapers

JPM na Museveni Wasaini Mkataba Ujenzi Mradi wa Bomba la Mafuta -Video

0

 

Rais John Magufuli wa Tanzania akitia saini mkataba wa mwisho wa utekelezaji wa ujenzi wa Bomba la kusafirishia mafuta Kutoka Uganda mpaka Tanzania leo.

Rais John Magufuli wa Tanzania na Rais Yoweri Museveni wa Uganda  leo  Septemba 13, 2020 wamesaini makubaliano ya kuanza ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga

Rais Magufuli amesema hatua hiyo ni ya muhimu sana kuelekea utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya takriban Dola za Marekani Bilioni 3.5

Rais Yoweri Museveni wa Uganda.


Ameongeza kuwa, hapa nchini bomba litapita kwenye Mikoa 8, Wilaya 24 na Kata 132. Aidha, watu zaidi ya 90,000 watalipwa fidia inayokadiriwa kufikia Bilioni 21

Rais Magufuli amempongeza Rais Museveni akisema amefanya mambo yasiyowezekana na endapo mafuta hayo yasingepatikana Uganda, Tanzania isingenufaika

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakiwa eneo la uwanja wa Ndege wa Chato. Mkoa wa Geita wakitia saini mkataba wa mwisho wa utekelezaji wa ujenzi wa Bomba lakusafirishia mafuta Kutoka Uganda mpaka Tanzania leo .
Rais Magufuli akiagana na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni Uwanja wa ndege wa Chato.

TAZAMA VIDEO CHINI

Leave A Reply