The House of Favourite Newspapers

FT: Yanga 3-0 Tanzania Prisons Uwanja wa Taifa, FA Cup

0

FULL TIME

Mwamuzi anapuliza kipenga kumaliza mchezo, Yanga inaibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Dakika ya 90: Muda wowote mchezo utamalizika, tayari ni dakika ya 93.

Dakika ya 90: Kamusoko anacheza failo katikati ya uwanja, anamsukuma kiungo wa Prisons. Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.

Dakika ya 88: Mohamed Samata wa Prisons anaambaa na mpira kulia mwa uwanjani lakini anapata uipinzani kutoka kwa Kessy.

Dakika ya 84: Mvua inaendelea kunyesha muda wote wa mchezo, kasi ya mpira imepungua.

Dakika ya 79: Yanga wanapata kona, ikiwa ni kona yao ya sita katika mchezo huu wa leo, wanapiga kona fupi lakini inaokolewa na walinzi wa Prisons.

Dakika ya 74: Kelvin Yondani anachezewa faulo na mchezaji wa Prisons wakati wa kuruka juu, anaumia jichoni na mchezo unasimama kwa muda, kisha unaendelea.

Dakika ya 72: Wachezaji wa Yanga wanapiga pasi vizuri lakini wanafika kwenye lango la Prisons wanajichanganya wenyewe na mpira unaondolewa.

Dakika ya 70: Yanga wanaendelea kutawala mchezo kwa kupiga pasi nyingi.

Dakika ya 62: Kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko anapiga shuti kutoka nje ya eneo la 18, mpira unatoka nje kabisa ya lango.

Dakika ya 60: Mchezo unaendelea kuwa na kasi huku mvua ikinyesha kwa wingi katika Uwanja wa Taifa.

Dakika ya 56: Anapiga penalti anakosa, mpira unagonga mwamba na kurejea uwanjani kisha walinzi wa Yanga wanaokoa.
Dakika ya 54: Prisons wanapata penalti baada ya nahodha wa Yanga, Nadir Haroub kumchezea faulo straika wa Prisons.

Dakika ya 51: Prisons wanafanya mabadiliko ya kipa, anaingia Aroun Kalambo, anatoka Andrew Ntalla ambaye ni kipa wa zamani wa Kagera Sugar na Simba

Hata kabla mchezo haujachangamka Msuva anafunga bao hilo kw ashuti kali kutoka nje ya eneo la 18, mpitra unaenda moja kwa moja wavuni licha ya kipa wa Prisons kuruka kwa ajili ya kuudaka.

Dakika ya 50: Yanga wanaendelea kushambulia kwa kasi

Yanga wanapata bao la tatu.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Kipindi cha pili kimeanza

MAPUMZIKO

Mwamuzi anapuliza kipenga kukamilisha kipindi cha kwanza, sasa ni mapumziko, Yanga inaongoza kwa mabao 2-0.

Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.

Dakika ya 44: Yanga wanacheza vizuri langoni mwa Prisons, Mwashiuiya anapata pasi nzuri ndani ya eneo la 18, anapiga shuti linatoka nje.

Yanga wanapata bao la pili.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dakika ya 33: Hassan Kessy wa Yanga anapata kadi ya njano kwa kumchezea faulo ya makusudi mchezaji wa Prisons.

Dakika ya 30: Yanga wanajaribu kuwatuliwa wapinzani wao kwa kupiga pasi kadhaa.

Dakika ya 28: Prisons wanapata nguvu baada ya kufungwa, sasa wanalishambulia lango la Yanga kwa nguvu.

Dakika ya 27: Prisons wanapata kona ya kwanza wakati Yanga wana kona tatu.

Dakika ya 24: Prisons wanafanya shambulizi kali, linapigwa shuti kali linagonga nguzo ya juu ya lango na kurejea uwanjani.

Dakika ya 18: Yanga wanaongoza bao 1-0, mchezo haujachangamka sana kutokana na uwanja kuwa na maji.

Dakika ya 16: Amiss Tambwe anaipatia bao Yanga wka kichwa baada ya kupokea krosi kutoka kwa Hassan Kessy

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!

Dakika ya 13: Yanga wanapiga kona lakini inaokolewa kwa kichwa na walinzi wa Tanzania Prisons.

Dakika ya 12: Simon Msuva anaingia na mpira langoni mwa Prisons, anapiga krosi nzuri lakini beki anaiokoa, mpira unatoka nje inakuwa kona.

Dakika ya 10: Yanga wanalisogelea lango la Prisons lakini wanashindwa kuwa na madhara.

Dakika ya 8: Yanga wanaendelea kutawala mchezo, idadi ya watu ni wachache kutokana na mvua.

Dakika ya 5: Timu zote zinashambuliana lakini Yanga ndiyo inamiliki mpira muda mwingi.

Dakika ya 1: Mchezo umeanza taratibu.

 

Mwamuzi anaanzisha mchezo. Mechi imeanza huku kukiwa na mvua inaendelea hapa kwenye Uwanja wa Taifa na maeneo mengi ya Dar es Salaam.

Timu zote zimeshaingia Uwanjani, mchezo utaanza muda si mrefu kutoka sasa. Ni mchezo wa Robo fainali ya FA Cup kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

KIKOSI CHA YANGA SC DHIDI YA TANZANIA PRISONS LEO ( ROBO FAINALI ASFC )
1. Beno Kakolanya
2. Hassani Kessy
3. Haji Mwinyi
4. Kelvin Yondani
5. Nadir Haroub
6. Juma Makapu
7. Saimoni Msuva
8. Thabani Kamusoko
9. Obrey Chirwa
10. Amisi Tambwe
11. Geofrey Mwashuiya

Akiba
– Deogratius Munishi
– Oscar Joshua
– Andrew Vicent
– Juma Mahadhi
– Antony Matheo
– Yusufu Mhiru
– Emanuel Martin

Mfumo : 4-4-2

Leave A Reply