The House of Favourite Newspapers

Makonda Amtaja Na Vee Money Ishu ya Madawa, Amtaka Kuripoti Kituoni Jumatatu

Vanessa Mdee ‘Vee Money’.

DAR ES SALAAM: Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemtaja na msanii wa Bongo Fleva, Vanesa Mdee ‘Vee Money‘ kuwa ni miongoni mwa wanaotuhumiwa kuhusika na mtandao wa biashara haramu ya madawa ya kulevya baada ya jina lake kuongezwa kwenye orodha iliyotajwa jana .

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wanahabari leo katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar wakati alipotaja majina ya watuhumiwa wengine wa madawa ya kulevya.

Makonda ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari wakati akitoa taarifa kuhusu kuitikia wito kwa wasanii 9 na askari polisi aliowataja jana kuhusika na biashara hiyo. Aidha Makonda amemtaka Vee Money kuripoti katika Kituo hicho Jumatatu ijayo kwa ajili ya mahojiano zaidi. Taarifa hiyo ilitolewa na Makonda katika ofisi ya Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishana Sirro, iliyopo sentro.

Makonda ameeleza kuwa ni watu watano tu ambao ni wasanii na raia wa kawaida ndiyo wameripoti leo kati ya wale waliotajwa jana. Mbali na hivyo, Makonda ametoa agizo kwa polisi kuwa, wale ambao hawajaripoti, watafutwe na wakamatwe hadi kufikia Jumatatu.

Save

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.