The House of Favourite Newspapers

NDALICHAKO Akizindua Ukumbi wa Mihadhara Chuo cha Mwl Nyerere – VIDEO

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amezindua ukumbi wa mihadhara wa kisasa katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere uliojengwa na mapato ya ndani ya Chuo hicho.

 

Akizundua ukumbi huo wa Mihadhara kigamboni jijini Dar es Salaam, Prof. Ndalichako amepongeza Bodi ya Utawala na Uongozi wa Chuo hicho kwa kusimamia vema matumizi ya fedha zinazotokana na Mapato ya ndani na kutumia kutekeleza miradi yenye tija kwa Chuo na Taifa kama ilivyofanyika katika ujenzi wa Ukumbi huo na pia amewataka uongozi kusimamia Dira na Dhima ya uanzishwaji wake kwa kujikita katika kutoa mafunzo ya Uongozi, Utawala na Maadili.

 

Prof. Ndalichako amewapongeza watendaji wa Chuo kwa kusimamia kwa karibu utekelezaji wa Mradi huo hadi kufikia hatua ya kukamilisha japo kwa kuchelewa kwa karibu miezi tisa.

 

“Nimefurahishwa na kazi hii nzuri iliyofanyika hapa, kwakweli ni jengo zuri lenye ubora wa hali ya juu na ambalo litawafanya wanafunzi kuongeza ari ya kujifunza na ninategemea kuona jengo hili likituzwa vizuri ili litumike kwa miaka mingi likiwa na ubora uleule” amesisitiza Ndalichako.

VIDEO: NDALICHAKO AKIFUNGUKA

Comments are closed.