The House of Favourite Newspapers

Yanga Wasonga Mbele Yawatoa Wolaitta Dicha Kwa Bao 2-1

Live: Wolaitta Dicha 1-0 Yanga SC, Kutoka Uwanja wa Hawass, Ethiopia

Timu ya Yanga wamesonga mbele kwa kuwatoa timu  ya Wolaitta Dicha kwa jumla ya bao 2-1

Katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam, Yanga ilishinda mabao 2-0 hivyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele katika michuano hiyo iliyo chini ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

Dk  90 zimeongezwa dakika +3

Dk 81  Wachezaji wa Wolaitta wanaonekana kukata tamaa

Dk 78 Wanashambuliana kwa kasi, Yanga wanaonekana kuongeza nguvu za mashambulizi

Dk 71 Mchezaji wa Yanga yupo chini

Dk  69 Yanga wanashambulia na kufanyiwa rafu nyingi refa anasema mpira uendelee

Dk ya 65 Yanga wanapata kona

Dk ya 64: Mashabiki wenyeji wanaongeza presha kwa Yanga kwa kushangilia muda mwingi.

Dk 63 Yanga wanashambukia kwa kasi sana

Dk 62 Wolaitta Dicha wanapiga kona kipa wa Yanga Youthe Rostand anaokoa

DK 58 Wolaitta Dicha wanakosa bao la wazi, mpira unatoka juu ya gori

DK  55 Wolaitta Dicha wanashambulia na Kipa wa Yanga Youthe Rostand anaokoa

Dk ya 52: Mchezo unaanza kuwa mkali.

DK 51 Yanga wanafanya mabadiliko anatoka Kamusoko ameingia Said Makapu

DK 48 Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi Yanga wanashambulia kwa kasi

HT: Wolaitta Dicha 1-0 Yanga SC

Dk ya 38: Tshishimbi anakosa nafasi ya wazi shuti lake linapaa juu ya lango.

Dk 33 Yanga wanashambulia kwa kasi, bao Yanga wapo nyuma kwa bao 1-0

Dk 29 Wolaitta Dicha wanakosa bao la wazi, mabeki wa Yanga wanajichanganya

Dk 27 Yanga wanapifa faulo kilometa chache kuelekea kwenye lanngo la Wolaitta Dicha

Dk 22 Bado timu ya Yanga ipo nyuma, Yanga wanashambuliwa sana na wanafanya kazi ya ziada ya kuokoa

DK  11 Yanga wanakosa bao la wazi Yussuf Mhilu, kipa anapangua

Dk ya 10 Yanga wanashambuliwa kwa kasi sana kipa wa yanga anafanya kazi ya ziada kuokoa

Timu zote zinashambuliana kwa zamu, mchezo una kasi

Wolaitta Dicha 1-0 wamepata bao dakika ya pili

Yanga wanaruhusu bao baada ya mpira wa kona kuwapita walinzi kabla ya kujaa wavuni.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 1. Dicha wanapata kona.
Mchezo unaanza kwa kasi.

Katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam, Yanga ilishinda mabao 2-0 hivyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele katika michuano hiyo iliyo chini ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

Kikosi cha leo cha Yanga @yangasc

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Kikosi kitakachocheza na Yanga

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Comments are closed.