The House of Favourite Newspapers

Liverpool Inarejea na Makali Yake 2020/2021

0

TIMU ya Liverpool inapewa tena nafasi kubwa ya kuhakikisha inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

 

Timu hii imekuwa bora kwa misimu miwili iliyopita ambapo imetwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu mmoja uliopita lakini msimu uliopita walifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England ikiwa imepita miaka 30 tangu walipoutwaa mara ya mwisho.

 

Hata hivyo, msimu huu timu hiyo inatakiwa kuwa bora sana na kuhakikisha kuwa inatumia tena uwezo wake kufanya mambo makubwa.Ili ifikie kwenye malengo yake, Liverpool wanatakiwa kuwa bora sana kwenye maeneo yafuatayo.

 

Nafasi msimu uliopita:1Walisubiri kwa miaka 30 kabla ya kumaliza ligi wakiwa kileleni na kutwaa ubingwa wao wa 19 kwenye historia ya timu hiyo.Klopp ameshasema kuwa ameandaa timu yake kwa ajili ya kufanya mambo makubwa kwenye msimu huu wa Ligi Kuu England akiwa anaaminika kuwa anaweza kuipa tena timu hiyo ubingwa.

 

“Msimu ujao hatu-na jambo lolote la kulinda, nafikiri utaku-wa msi mu mp ya na kazi yetu itakuwa kushambulia tu.

“Sioni kama kuna jambo ambalo nimelipata hadi sasa, nafikiri tupo katikati na tunatakiwa kuhakikisha tunapambana sana kuwa bora zaidi ya hapa tulipo.

 

“Tunaandaa timu kwa ajili ya kutwaa ubingwa na siyo jambo lingine, kitu pekee ambacho mashabiki wanatakiwa kukisubiri kutoka kwetu ni mafanikio ya msimu huu.

“Nafikiri wengine wanakumbuka kuwa tulitwaa ubingwa tukiwa na michezo saba mkononi na pia hatujafungwa kwenye Dimba la Anfield kwa miaka mitatu, lazima tuendeleze haya mazuri kwenye timu yetu.

 

“Liverpool walimaliza Ligi Kuu England wakiwa na pointi 18 na kuwa kati ya timu iliyomaliza msimu wa ligi ikiwa na pointi nyingi zaidi,” alisema Klopp.Liverpool walitwaa ubingwa wakiwa na safu bora ya ulinzi ambapo walinzi wake akiwemo Trent Alexander-Arnold na Andy Robertson, walifanya mambo makubwa sana kwenye ligi hiyo.

 

Ambapo kiungo wa Manchester City, Kevin De Bruyne ndiye pekee aliyeonekana kuwa bora kwenye kutoa pasi za mabao kuliko beki huyo wa pembeni wa Liverpool.Timu hii ilionekana kuwa bora sana kuliko nyingine zote kwenye ligi hiyo ikiwemo Manchester City, Chelsea na Manchester United ambazo zilimaliza ligi zikiwa kwenye nne bora.

 

NYOTA WAO MSIMU HUU

Bado safu ya ulinzi ya Liverpool inaonekana kuwa bora chini ya beki Virgil van Dijk, msimu uliopita Van Dijk alicheza kila dakika kwenye timu hiyo, bado anaonekana kuwa anaweza kuwa staa zaidi msimu huu.

 

Vijana wachanga:Bado timu hiyo inatarajiwa msimu huu kuwika na baadhi ya wachezaji vijana, akiwemo Rhian Brewster ambaye msimu uliopita alifanya mambo makubwa akiwa na Swansea. Brewster alifanikiwa kufunga mabao 11 kwenye michezo 22, aliyoitumikia timu hiyo, na sasa anaonekana kurudi kwenye timu yake.

 

INGIZO JIPYA

Liverpool kwa sasa wanamwinda Thiago Alcantara kutoka kwenye kikosi cha Bayern Munich ingawa mwenyewe amekiri kuwa hana mpango wa kuondoka hapo.

 

Klopp pia anatakiwa kuhakikisha kuwa anapata msaidizi wa Andy Robertson kwa ajili ya msimu huu ambao unaonekana utakuwa mgumu sana kwa timu hiyo.Mwingine ambaye anawindwa na Liverpool msimu huu ni Mgiriki Jamal Lewis ambaye anatajwa kuwa kati ya wachezaji bora zaidi kwenye soka la sasa.

Leave A Reply