The House of Favourite Newspapers

Lori lililobeba Sumu ya Sodium Cyanide Ya Migodini Lapata Ajali Kahama

0
Gari aina ya scania lenye usajili  wa namba T124 ECX linalobeba sumu  ya sodium cyanide inayapeleka Migodi mitatu nchini limepata ajali eneo la Kagongwa  Wilaya ya Kama na sumu hiyo kumwagika.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 3:00 asubuhi ambayo ilizua taharuki kubwa kwa wananchi wa eneo hilo ambapo wananchi hao walipewa tahadhari wasisogee eneo la tukio  kwani kuna hatari  na wakae mbali kuepusha madhara.
Akizungumza leo Oktoba 17 Wilaya ya Kahama baada ya kufika kwenye tukio hilo  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP, Janeth Magomi amesema alipata taarifa majira ya saa 3:20 asubuhi kuwa gari la Kampuni ya Taifa Transport & Logistic limedondoka  katika Kata ya Kagongwa Wilaya hiyo na hivyo akaenda eneo tukio.
Amesema vyombo vya usalama  vinaendelea na udhibiti  kuepusha madhara  kwa wananchi na hivyo ni  lazima tahadhari ziwepo kwa sababu  sumu ni hatari.
“Nilivyofika kwenye eneo la  tukio ni kweli ajali  imetokeoa na huduma za uokaji  zinaendelea ambapo dereva mmoja kati ya madereva kumi waliokuwa wakisafirisha sumu ya sodium cyanide amepata ajali na kapewa huduma na kuhakikisha madhara hayotokei kwa wananchi, ” amesema Kamanda Magomi.
Amesema  dereva huyo amepewa huduma  ya kwanza  kutoka kwa waaguzi  na anaendelea  vizuri.
Amesema  amewasisitiza  wananchi  waendelee kutoa taarifa kwa jeshi la polisi  wanaopoona matukio  ya aina hiyo na hawasogei eneo hilo kwa tahadhari hadi sasa hakuna  madhara yeyote.
Aidha amesema hali ni shwari na amewatoe wasiwasi  wananchi  wote wa eneo hilo waaendelee na shughuli zao za kila siku na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama.
Naye Mkuu wa Jeshi la  Zimamoto na Uokoaji  na Mkaguzi wa Wilaya  ya Kahama, Edward Selemani amesema  wao wamejianda kufanya uokaji muda wowote mara tu tukio linapotokea.
Amesema  walivyopokea taarifa za tukio hilo walijiandaa kwa kuvaa vifaa vya uokozi na kuhakikisha sumu ya sodium cyanide  isilete madhara kwa wananchi.
“Wananchi kuwa na tahadhari kubwa matukio kama haya yanapotokea na wasisogelee eneo hili kwa sababu sumu ni hatari na unaweza kupoteza maisha,”amesema Selemani.
Naya Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa Mtaa wa Kashime, amesema  walipata mshituko  kuona tukio la ajali  hiyo.
“Ajali hii imetuogopesha  tulikuwa na taharuki  maana gari limeandikwa hatari na sumu, tumeona dereva anadondoka  baada ya muda tukaona watu wanahangaika na kutoa huduma ya kwanza ikabidi tukae mbali na eneo hili ,”amesema Mabula.
Kwa upande wake  Meneja  wa Mradi  wa Kampuni ya Taifa  Transport &Logistic,  Happiness Nyiti amesema  amepokea taarifa za ajali akiwa kwenye Mgodi wa Buzwagi na hivyo  ikambidi afike kwenye eneo la tukio.
“Ni kweli ajali iliyotokea ni gari ya kampuni yetu gari aina ya scania lenye usajili wa namba T124 ECX linalobeba sumu  aina ya sodium cyanide inayopelekwa kwenye migodi ya Buzwagi,  Bulyankulu na North Mara,”amesema Nyiti.
Amesema kwanza anashukuru vyombo vya usalama na wadau  kwa kuweza kudhibiti ajali hiyo hadi sasa hakuna madhara  yeyote yaliyotokea kwa wananchi na hali ya dereva anaendelea vizuri kwa sasa.
Aidha amesema  wanafanya mafunzo ya madereva wote wanaoendesha magari yanayobeba sumu ya sodium cyanide.
“Mafunzo hayo  yanatolewa na Ofisi ya Mkemia Mkuu  wa Serikali  na kupewa vyeti kwaajili ya kusafirisha sumu ya sodium cyanide na tunahakikisha  wakiwa safarini madereva wana vifaa vya kujikinga na sumu hizo ikiwepo mbele convoy leader na escot,”ameongeza.
Leave A Reply