Kartra

Luis, Saido Watu wa Kuchungwa Kariakoo Dabi

KUELEKEA mchezo wa Kariakoo Dabi kati ya Simba dhidi ya Yanga, guu la kulia la nyota wa Yanga, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ ni la kuchungwa na wapinzani wake Simba kwa kuwa limekuwa na maajabu kila awapo uwanjani.

 

Akiwa amehusika katika jumla ya mabao 9 kati ya 49 yaliyofungwa na timu hiyo msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara, amefunga mabao manne na kupiga asisti tano.

Kwa guu la kulia, amefunga mabao yote hayo na kupiga asisti tatu, huku guu la kushoto akitumia kupiga asisti mbili.

 

Upande wa Simba, mtu wa kuchungwa zaidi ni Luis Miquissone anayetumia zaidi guu la kushoto ambalo limefunga mabao saba, huku guu la kulia akifunga moja na kichwa moja. jumla amefunga mabao tisa na kutoa asisti kumi.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA, DAR ES SALAAM


Toa comment