The House of Favourite Newspapers

LUKUVI: ‘ZEGE HAILALI’ ATOA SIKU 60 WAMILIKI WA VIWANJA DAR

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametoa siku 60 kwa wamiliki wa viwanja vilivyopimwa kuviendelezwa ili kuzuia migogoro ya ardhi.

 

Lukuvi amesema hayo leo katika viwanja vya Shule ya Bunju A alipokutana na wananchi wa wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi iliyopo wilayani humo ambapo amesema zoezi la upimaji wa viwanja takribani 20,000 limekamilika na kuwataka wananchi kuviendeleza.

 

Akizungumza katika mkutano huo wa hadhara ambapo aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Lukuvi amesema endapo viwanja hivyo havitaendelezwa viwachukuliwa na halmshauri ili wapewe wenye uwezo wa kuviendeleza.

Lukuvu aliyasemahayo baada ya Makonda amesema Kinondoni ni moja ya wilaya zenye migogoro ya ardhi iliyokosa ufumbuzi kwa muda mrefu hivyo alimuomba Waziri asikilize kero za wananchi na kuzitolea maamuzi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwapa maelekezo wakazi wa Wilaya ya Kinondoni waliofika katika Viwanja Vya Shule ya Msingi Bunju kutatuliwa kero zao za ardhi.

 

Alisema  migogoro yote hiyo ni ya miaka mingi iliyopita ambayo ilichangiwa na wananchi wengi kutokuwa na hati.

 

Ameeleza kuwa kwa sasa hakuna mwananchi atakayemiliki hati kinyemela na badala yake atamiliki hata zaidi ya ekari 50 kwa kufuata sheria na kuwa na kitambulisho cha taifa kutoka NIDA kitakachokuwa katika mfumo wa kidijitali kueleza taarifa rasmi za mmiliki.

Mabango yenye ujumbe mbalimbali yakitawala.

 

Aidha, viongozi hao wametumia kauli ya mafundi ujenzi inayosema ‘zege hailali’ ili kuhakikisha  wanasikiliza na kutatua kero za wananchi wa wilaya ya Kinondoni hata kama itafika usiku wa manane.

Katika zoezi hilo, Makonda amewaomba wananchi kutoa ushirikiano pale watakapoanza kusikilizwa kero zao kupitia kwa waziri Lukuvi kutokana na baadhi ya kero kuhitaji vielelezo zaidi kwa pande zote husika.

Waziri Lukuvi yupo kwenye ziara ya siku tano katika mkoani Dar es Salaam ili kutatua migogoro ya ardhi iliyopo katika wilaya za mkoa huo.

Comments are closed.