The House of Favourite Newspapers

Tarehe ya Hukumu ya Tido Muhando Yatajwa

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Januari 25, 2019,  kutoa hukumu ya kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando.

 

Hukumu hiyo ilipangwa kusomwa leo Jumanne Desemba 18, 2018 lakini Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Huruma Shaidi,  amesema hajakamilisha kuandaa hukumu kwa sababu kuna vitu bado anavifanyia utafiti kabla ya kutoa hukumu hiyo.

 

“Hukumu yako Tido bado haijakamilika, kuna vitu bado navifanyia utafiti. Januari 25 nitatoa hukumu, hivyo utaendelea kuwa nje kwa dhamana hadi siku hiyo,” amesema Hakimu Shaidi.

 

Tido anakabiliwa na mashtaka matano, mashtaka manne ni ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia serikali hasara ya Sh. milioni 887.1.

Comments are closed.