Lulu Atoa Povu la Mimba!

MUIGIZAJI mwenye vituko lukuki Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kwa kuwa watu wengi wamekuwa wakimuuliza kuhusiana na mimba yake basi akiibuka tena atakuwa amebeba kichanga ili kuwaziba midomo wananzengo.

Akizungumza na Za Motomoto News, Lulu alisema picha yake inayomuonesha akiwa na kitumbo iliyosambaa mitandaoni imewatoa povu watu wengi, sasa hajui wakimuona na mtoto watasemaje.

“Jamani mimba kila mtu ilimuinua mishipa ya shingo sasa ni hivi, nikionekana tena kwenye mtandao au popote nina mtoto wangu mikononi sasa hapo sijui watasema lugha gani kwa kweli,” alisema Lulu bila kufafanua kwa undani kama ni kweli ni mjamzito au la.

Stori: Imelda Mtema

Toa comment