The House of Favourite Newspapers

Rasmi Matola Kocha Msaidizi Wa Simba, Aanza Na Mkwara Huu

0

SELEMAN Matola, ametangazwa kuwa Kocha Msaidizi wa Simba leo akipokea mikoba ya aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo.

 

Matola amesema kuwa amerejea nyumbani na anaamini kwamba atafanya kazi kwa ukaribu kutokana na uzoefu alionao.

“Nimerejea nyumbani na nina imani ya kufanya vema, nahitaji sapoti kwa mashabiki kutokana na kutambua vema falsafa ya Simba.

 

“Nilikuwa ndani ya Simba kwenye timu ya vijana kwa sasa nitaendelea gurudumu kwa kushirikiana na benchi la ufundi,” amesema.

 

Matola alikuwa kocha wa Polisi Tanzania alivunja nao mkataba wake wa mwaka mmoja baada ya kufika makubaliano mazuri na uongozi wa Simba na kwa sasa Polisi Tanzania ipo chini ya Malale Hamsini.

Leave A Reply