The House of Favourite Newspapers

LULU DIVA AWEKA WAZI ‘WEUPE’ WAKE

0

 

MSANII wa kike wa muziki wa Bongo Fleva nchini Lulu Diva, ameweka bayana siri ya weupe wake.
Mwanamuziki huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Give To Me’ na anaendelea kupambana na muziki wa kisasa.

 

Akiongea na redio moja hapa nchini, Lulu Diva amefunguka haya: “Msanii unatakiwa unaanza kujibrand kuanzia mwili, ngozi yako na vitu unavyokula. Naweza nikasema mimi nakula sana mboga za majani na matunda, pia kuna baadhi ya vyakula vinasaidia sana ngozi kung’ara ,” amesema Lulu Diva

 

Katika hatua nyingine msanii huyo amezungumzia kolabo yake na ExQ kutoka nchini Zimbabwe na kueleza msanii huyo ndiye aliyemtafuta.

 

“Ndiyo kolabo ya kwanza kushirikishwa tena kutoka nje ya nchi, ina maana kwamba wameona Lulu anaweza kufanya kitu kikubwa. Ndo mana wameniamini,” amesema msanii huyo wa muziki.

 

NA : SAMSON JEREMIAH/GPL

Leave A Reply