The House of Favourite Newspapers

Lulu Diva: Jela ni Shule

STORI: Na IMELDA MTEMA| RISASI JUMAMOSI|DAR ES SALAAM

KUFUATIA kuonja joto la sero kwa siku kadhaa, msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbasi ‘Lulu Diva’ ameibuka na kusema sero ni shule kwani amejifunza mambo mengi.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Lulu Diva alisema kwenye maisha yake hakuwahi kutegemea kuingizwa sero lakini kwa muda aliokaa, amepata uzoefu mpya ambao hatausahau maishani mwake.

“Yaani mle ndani kwangu mimi kila kitu kilikuwa kigeni, mazingira yalivyo, watu waliomo mle kwa kweli si mahali pa kuomba au kutamani kwenda, nimejifunza kwa kweli,” alisema Lulu Diva.

Msanii huyo pamoja na wenzake ambao walihusishwa na madawa ya kulevya, waliachiwa kwa kiapo maalum cha mahakama, Jumanne iliyopita ambapo watakuwa chini ya uangalizi maalum wa jeshi la polisi.

 

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Save

Comments are closed.