Lulu Diva: Ugomvi na Nandy ni Utoto

MSANII wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amesema ugomvi unaodaiwa ulikuwepo kati yake na msanii mwenzake Faustina Mfinanga ‘Nandy’ ni wa kitoto tu.

 

Akizungumza na Risasi Vibes, Lulu Diva amesema siku zote panapokuwepo wanawake zaidi ya wawili, hakukosekani maneno ya hapa na pale, hivyo ndiyo maana kukatokea ‘kaugomvi’ ambako hata hakakuwa na msingi wowote.

 

“Sidhani kama nilikuwa na ugomvi wa maana kati yangu na Nandy, yaani ni ugomvi tu wa ki-mwanamke, hauna maana yoyote na pia hakuna kitu kibaya kama maneno ya kuambiwa, hivyo niko vizuri tu na Nandy na haipendezi kioo cha jamii kugombana hovyo,” alisema Lulu Diva bila kufafanua kwa undani chanzo cha ugomvi huo.

 

Kwa siku za karibuni, wawili hao walikuwa kwenye sintofahamu huku chanzo kikiwa hakifahamiki kwa undani.

 STORI | Imelda Mtema, Risasi

Toa comment