The House of Favourite Newspapers

Lusajo Awapa Masharti Yanga ili Asaini

0

RELLIANTS Lusajo, mshambuliaji wa Namungo FC, amesema iwapo Yanga au Simba zinahitaji saini yake, ni lazima ahakikishiwe kucheza kikosi cha kwanza na maslahi bora ili asaini.

 

Habari zinaeleza kuwa nyota huyo ambaye ni nahodha, anahitajika zaidi ndani ya klabu yake ya zamani ya Yanga ambayo ina ubutu kwenye safu ya ushambuliaji ikiwa imecheza mechi 27 imefunga mabao 31 na kinara wao ni David Molinga mwenye mabao nane.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Lusajo alisema kuwa amekuwa akisikia taarifa za yeye kuhitajika na klabu hizo kubwa, jambo ambalo halimpi presha, ila ili asaini lazima utaratibu uzingatiwe.

 

“Ninatambua kwamba kuna timu ambazo zinanihitaji, mimi ni mali ya Namungo lakini ili niweze kusaini ni lazima nitazame nafasi yangu ya kucheza kikosi cha kwanza pamoja na maslahi, ndiyo vitu muhimu.

 

“Ninajiamini katika kazi yangu, ndiyo maana nikiwa uwanjani ninafunga, ikishindikana ninatoa nafasi za kufunga kwa wengine, sina mashaka,” alisema Lusajo.

 

Namungo ikiwa nafasi ya nne na mabao yake 34 kibindoni, amehusika kwenye mabao 14 ambapo amefunga 11 na kutengeneza nafasi tatu za mabao.

Leave A Reply