The House of Favourite Newspapers

Lwandamina aitangazia vita Zanaco

Omary Mdose | CHAMPIONI| Dar es Salaam

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina, amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wao wa kesho Jumamosi dhidi ya Zanaco licha ya kufahamu kwamba hawakuwa na matokeo mazuri kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa hapa nyumbani.

Yanga ambayo jana Alhamisi iliondoka hapa nchini kuelekea Zambia kwa ajili ya mchezo wa marudiano, ilitoka sare ya bao 1-1 na Zanaco, Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Lwandamina ambaye alikuwa kocha wa Zesco ya Zambia kabla ya kujiunga na Yanga, Novemba, mwaka jana, ameliambia gazeti hili kuwa, katika soka hakuna nyumbani wala ugenini, hivyo wanakwenda Zambia kuhakikisha wanafuzu hatua inayofuata.

“Huwezi kusema umetolewa mashindanoni au umefuzu baada ya matokeo ya mchezo wa kwanza, bali matokeo ya jumla ndiyo siku zote hutoa majibu ya kweli.

“Sare ya hapa nyumbani haimaanishi kwamba hatuna nafasi tena ya kusonga mbele, tumejiandaa kwenda kupata matokeo mazuri ili tusonge mbele kwa sababu lengo letu ni kuona tunacheza hatua inayofuata na kufika mbali kwenye michuano hii,” alisema Lwandamina.

Comments are closed.