The House of Favourite Newspapers

Beyonce Kupata Mapacha wa Kiume!

Beyonce Knowles

Na MWANDISHI WETU| GAZETI LA IJUMAA|SHOWBIZ MAMTONI

IMEBAINIKA kuwa mwanamuziki wa R&B asiyechuja, Beyonce Knowles huenda akajifungua mapacha wa kiume kutokana na ishara mbalimbali anazozionesha.

Hivi karibuni Beyonce aliweka picha katika tovuti yake ya ukurasa wake wa Instagram ikimuonesha akiwa katika kigauni cheusi cha kubana huku eneo la juu akiwa amevalia hereni kubwa za silva ambazo amewahi kuzivaa katika video yake ya mwaka 2008 ya Wimbo wa If I Were A Boy jambo linaloonesha huenda kweli akapata mapacha wa kiume.

Japokuwa hadi sasa Beyonce na mumewe Jay Z ambao wana mtoto mmoja, Blue Ivy bado hawajatoa tamko lolote juu ya jinsi ya mapacha hao lakini watu wa karibu na mastaa hao wanasema kuwa kiu kubwa ya mwanamama huyo ni kupata mapacha wa kiume.

 

Comments are closed.